Menu
 

Bwana JUMA GTAT, wachezaji wengine watatu wa timu ya taifa, na kocha wa timu kuu ya Tripoli al-Ahly, Adel bin Issa wamejiunga na Kundi la Waasi ambalo linapigana vikali na Serikali ya MUAMMAR GADAFI kupigania haki na Maslahi ya wana - Libya..


GTAT unayaweza haya sio sawa na Kudaka Mpira!!
Bwana GTAT akitoa mchango wake.
Juma Gtat, golikipa wa timu ya taifa ya Libya na kocha wa al-Ahly, Adel Issa


Uongozi wa waasi mashariki mwa Libya umesema kuwa wachezaji 4 wa timu ya taifa ya kandanda ya Libya, wamejiunga na waasi wanaopigana dhidi  ya kanali Muammer Gaddafi.

Naibu mwenyekiti wa baraza la waasi, Abdel Hafiz Ghoga, amesema wachezaji hao na maafisa wengine 13 wa kandanda wanaishi katika nchi jirani ya Tunisia.

Miongoni mwa waliojiunga na waasi hao anadhaniwa kuwa ni  mlinda  mlango  wa timu hiyo ya taifa na kocha wa timu moja  kubwa  ya kandanda nchini humo. Siku moja kabla, waasi hao walisema wanafanya mazungumzo yasio ya moja kwa moja na utawala, kuhusu uwezekano wa makubaliano ya kisiasa  ambapo Gaddafi atajiuzulu. Wakati huo huo shirika la kujihami, NATO, limekana  kuwa limewaua raia 15 katika mashambulio katika mji uliopo mashariki, Brega katika  saa 24 zilizopita, kama ilivyodaiwa na utawala wa Gaddafi. Msemaji mmoja wa NATO alikiri kuwa majengo yalishambuliwa katika eneo hilo, lakini amesema maeneo hayo yalikuwa yamelengwa kikweli kijeshi.
 

Post a Comment

 
Top