Menu
 

 
Abbas Abdallah (31), mkazi wa Kijiji cha Kiru Ndogo, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara ambaye amevimba mguu, jana alianza kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mjini Moshi.

Kijana huyo alisafirishwa juzi kutoka kijijini kwake kwenda Hospitali ya Seliani, mkoani Arusha kwenda kupata matibabu, lakini  madkatari wa hospitali hiyo walishauri apelekwe Hospitali ya KCMC.

Kwa sasa anayetaka kumsaidia kijana huyo awasiliane kwa namba 0786 272409 au 0655 304336....
MNYIKA ATAKA WAZIRI NGELEJA ABANWE MGAWO WA UMEME.

 
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amewaomba wabunge wote kuibana na kuiwajibisha serikali wakati wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itayowasilishwa keshokutwa ili kupata mwelekeo wa ufumbuzi wa tatizo la mgawo wa umeme. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mnyika alisema serikali imeendelea kutoa majibu yenye kukatisha tamaa kuhusu namna ambavyo inashughulikia tatizo la mgawo wa umeme na upungufu wa gesi asilia.

Alisema kama serikali haitotoa majibu kwa kambi ya upinzani bungeni, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kitawaongoza Watanzania kuunganisha nguvu ya umma kupitia maandamano kuishinikiza serikali kuchukua hatua za haraka kupunguza mgawo mkubwa wa umeme na upungufu wa gesi asilia unaondelea hivi sasa. “Leo (jana), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ametoa majibu yenye kuthibitisha kwamba serikali inaendelea kuachia mgawo huu mkubwa wa umeme na upungufu wa gesi asilia uendelee kwa muda mrefu zaidi.

Hivyo, ni muhimu kusisitiza kwamba Waziri wa Nishati na Madini na Naibu wake wanapaswa kujiuzulu kwa hasara ambayo inaendelea kulikumba taifa kutokana na mgawo huu na upungufu wa gesi asilia unaondelea ambao umesababishwa na uzembe na udhaifu wa kiuongozi,” alisema.

Alisema serikali kupitia kwa Rais Jakaya Kikwete, katika hotuba yake kwa taifa ya Aprili Mosi, mwaka huu, iliwahakikishia Watanzania kwamba kuanzia Julai taifa litapata mitambo ya dharura ya megawati 260.

Alisema mitambo hiyo ya dharura ambayo inaingiza gharama kwa serikali ni matokeo ya uzembe na udhaifu wa kiuongozi uliotokana na kuchelewa kufanya ununuzi wa mitambo ya umeme ya MW 100 Ubungo na MW 60 Mwanza ambayo hapo awali ilipangwa ikamilike mwaka 2010.
KAMPUNI YA SIMU YA MKONONI YA VODAFONE YA UINGEREZA YAFANYA ZIARA YA CCBRT.


Muuguzi wa Hospitali ya CCBRT kitengo cha wagonjwa wa Fistula, Emelda Lweno akimwonesha mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Huduma kwa Jamii wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza, Elizabeth Filkin wanawake wenye ugonjwa huo ambao matibabu yake yanafadhiliwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania wakati wa ziara yake hospitalini hapo.
 Kwa mujibu wa mtandao wa.....
http://chingaone.blogspot.com/

Post a Comment

 
Top