Menu
 

 
Benki ya CRDB tawi la mbeya imetoa mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 300 kwa wakulima wadogowadogo wa chai wa wilaya ya Rungwe ili waongeze uzalishaji wa zao hilo.

Hayo yamebainika wakati wa uzinduzi wa ofisi ya chama cha akiba na mikopo SACOSS cha wakulima hao.

Kaimu meneja wa benki hiyo JOHNSON MWANSOJO amesema kuwa mkopo huo utaiwezesha SACOSS hiyo kutoa huduma za kibenki.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kata ya Kandete mwakaleli MWANSOJO amesema mkopo huo utanufaisha wakulima wazao wapatao elfu 15.

MWANSOJO amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa tawi hilo ni kuwajengea uwezo wakulima kupata fedha zao za malipo ya mazao ya kilimo na kuwaepusha kutembea umbali mrefu kutafuta malipo hayo.

Amesema hiyo ni mikakati ya CRDB kuhakikisha inawajengea uwezo wakulima na kujikita zaidi katika uzalishaji wa chai na kuwawezesha kupata mikopo kwa uraisi kupitia SACOSS yao ili kujikwamua na umaskini


WALIMU WAJIUNGA NA SACCOS MBEYA.
Walimu wapya 243 wamejiunga na chama cha mfuko wa uwekezaji wa fedha (teachers saccos Mbeya)


Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti wa chama hicho Anna Mwakalukwa wakati wa mkutano wa wanachama hicho na kuwataka waalimu kujenga ushirikiano wa pamoja ili kukijenga chama hicho.

Amesema kupitia mikopo wanayoitoa waalimu wameweza kupata maendeleo kwa kuanzisha biashara ndogondogo ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba.
 NZOVWE JIJINI MBEYA


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka wakazi wa kata ya Nzovwe kutochangia shughuli zozote za maendeleo katika kata hiyo kutokana na kujiuzuru kwa Diwani wa kata Hiyo Hezron Mwakalobo.

Msimamo huo umetangazwa na Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala, katika mkutano wa chama hicho uliofanyika kata ya Nzovwe kwa lengo la kueleza sababu za kujiuzuru kwa diwani wao.

Mwamalala amesema viongozi wa CCM wameanzisha mpango wa kuwarubuni madiwani wa chadema wajiunge CCM ikiwa ni pamoja na kujiuzuru nyadhifa zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John Mwambigija, amesema diwani Hezron Mwakalobo aliyejiuzuru anapaswa kuwaomba radhi wananchi wa kata ya Nzovwe waliomchagua kwa kuwasaliti kutokana na kuhongwa fedha ili ajiunge na CCM.

Nao madiwani wa Chadema wamesema kuondooa kwa Hezron Mwakalobo ni faraja kwao kutokana na yeye kuwa mzigo katika mikutano ya baraza la Halmashauri ya jiji.

Post a Comment

 
Top