Menu
 


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya ADVOCATE NYOMBI amesema jeshi lake linaendea na uchunguzi ili kubaini ukweli wa mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya dhidi ya mwekezaji wa kampuni Rice Project

Kuhusu vitendo vya uharibifu wa mali za wananchi Kamanda NYOMBI amesema hana taarifa nazo na kwamba na kuwataka  wananchi hao kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea.

Hata hivyo habari tulizozipata zinadai kuwa mwekezaji huyo alivunja matofali kumi na mbili elfu ambayo yalifyatuliwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Mbarali na kumjeruhi mwanakijiji kwa kumgonga na gari.

Post a Comment

 
Top