Menu
 

Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani mbeya imemkamata  Hakimu Mfawidhi   wilaya ya Mbozi  Ndugu Nyagesa Kajanja  miaka (30) na mwenzake  Zenna Mwakamela (30) kwa kosa la kuingiza bidhaa nchini kinyume na utaratibu .

Imeelezwa kuwa  watuhumiwa hao walikamatwa   katika eneo la Iwambi jijini mbeya  katika  barabara ya Mbeya Tunduma wakiwa na bidhaa hizo ndani ya gari  T 999 BDK  wakati maofisa  hao wa TRA wakiwa katika msako .

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake Kamanda wa Polisi mkoani humo Advocate Nyombi amesema mara baada kukamatwa  kwa mtuhumiwa huyo  alifikishwa katika kituo cha polisi jijini mbeya kwa lengo la kutoa maelezo juu ya tukio hilo.

 Amesema kulingana maelezo ya maofisa wa TRA wanadai kuwa mtuhumiwa alikamatwa na  sabuni za kufulia aina ya Boom mbazo  hazijalipiwa ushuru pamoja na bidhaa ambazo zinadaiwa kupigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.

Nyombi amesema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea na mtuhumiwa amefikishwa katika mahakama  ya wilaya ya Mbeya.Kufuatia taarifa za maofisa wa TRA zinadai kuwa mtuhumiwa huyo aliwahi kukamatwa na kosa hilo la kuingiza bidhaa nchini kinyume cha sheria  na kufikishwa mahakamani ambapo mpaka kipindi hiki cha kukamatwa kwake mtuhumiwa bado alikuwa na kesi ya kujibu licha ya kukutwa na kosa jingine ambalo amelitenda Julai 14 make huu.

Mbali na hilo Kamanda Nyombi amesema jeshi la polisi mkoani humo limefanikiwa kukamata silaha iliyotumika katika tukio la ujambazi wilayani Kyela katika eneo la mikumi  na kufanikiwa kupora zaidi ya shilingi milioni  150 ambazo ni mali ya kampuni ya ufununuzi Kokoa( BIOLAND).Amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendeklea na watuhumiwa watatu wamefikishwa mahakamani .

Post a Comment

 
Top