Menu
 
Msemaji wa Kamati Maalumu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Boniface Benezeth, akisoma taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), leo mchana jijini Dar es Salaam, kuhusu mgomo wa wanafunzi wa chuo hicho uliofanyika hivi karibuni
KAMATI MAALUMU YA WANAFUNZI WA TAASISI YA USTAWI WA JAMII
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu Wanahabari,
JULAI 21, 2011, Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) ilisitisha masomo (kufunga chuo) kwa muda usiojulikana kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni mgomo usio halali wa wahadhiri. Hali hii ya kufunga chuo (kusitisha masomo) imekuwa na madhara makubwa kwa wanafunzi (wanachuo) ikiwa ni pamoja na wengi kukosa malazi na hata wengine kushindwa kujikimu kimaisha huku wengine muda wao wa ruhusa kazini ukimalizika.
Kutokana na hali hiyo, baada ya tangazo la kusitisha masomo kutolewa na Kaimu Mkuu wa Taasisi, Mlwande Madihi mbele ya Mkutano Mkuu wa Wanafunzi ikiwa yapata saa 11:15 jioni, wanafunzi wote wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii katika Mkutano huo wakiongozwa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi (ISWOSO) walikubaliana na kuunda Kamati Maalumu ya Dharura kwenda Dodoma kuwasilisha kilio cha wanafunzi kwa Serikali na hasa ikizingatiwa kuwa kutokana na vikao vya Bunge la 10 kuendelea, wakiamini kuwa viongozi hao wa Serikali (Mawaziri na Manaibu Waziri) watapatikana kirahisi hukohuko.
JULAI 24, 2011 (Jumapili), Kamati ilifika Dodoma na ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Chrisant Mutatina; Makamu Mwenyekiti Mariam Saad na Katibu Kitamogwa Safari. Ikiwa Dodoma, ilikutana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na kisha ikakutana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya.
Siku iliyofuata Kamati hiyo ikiwa na wajumbe 10 ilikaribishwa katika Kikao cha Bunge na Mheshimiwa Idd Azzan ambaye ni Mbunge wa Kinondoni (CCM) ilipo Taasisi yetu ya Ustawi wa Jamii pamoja na Mheshimiwa Mwiguru Lameck Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM).
Kamati iliyoundwa na Mkutano Mkuu ilikuwa na wajumbe ambao ni pamoja na Gerald J. Simbeya (Rais wa ISWOSO), Boniphace Benezeth, Khadija Mkwama, Tatu Said, Joseph Sabinus, Godfrey Kinogo (Waziri wa Mikopo- ISWOSO), Johnson Rutechula, Julieth Muchunguzi, Machibya Mayala na Kenan Edwin. Hata hivyo, Simbeye (Rais), Tatu Said na Kenan Edwin walishindwa kufika Dodoma kwa sababu mbalimbali zikiwamo za kifamilia.
Alhamisi ya Julai 28, 2011, Kamati hiyo ilikutana na kuzungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Hussein Mponda. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Bunge yakiwahusisha waheshimiwa Wabunge Idd Azzan na Mwiguru L. Nchemba.

Katika mazungumzo hayo kwa nyakati tofauti, Kamati iliwaeleza Mawaziri wote wawili (Dk. Mponda na Dk. Kawambwa) na Naibu Waziri (Dk. Nkya) kuwa baadhi ya watu kwa maslahi binafsi wamejaribu kupotosha ukweli wakisema wanafunzi waligoma ingawa ukweli ni kwamba walifanya Mkutano Mkuu halali ulioitishwa Jumatano (Julai 20) na Rais halali wa Serikali ya Wanafunzi (ISWOSO), Gerald Julio Simbeye na kuahidiwa kuwa siku iliyofuata yaani Alhamisi ya Julai 22, saa 4:00 asubuhi wangepewa majibu kuhusu adha na kilio chao cha ukosefu wa walimu (kukosa masomo) kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Taasisi.
Ndipo katika hali ya kushangaza siku hiyo ya Alhamisi Julai 21, 2011 badala ya kupata majibu hayo, wakapewa tangazo la kufunga Chuo kwa muda usiojulikana kwa kilichotajwa kuwa ni kutokana na mgomo usio halali wa wahadhiri na kutakiwa kuondoka mara moja.
TUNAPENDA UMMA UTAMBUE UKWELI KUWA:-
1. Mkutano wa wanafunzi ulifanyika siku moja na wakaahidiwa kupewa majibu siku ya pili saa 4:00 asubuhi hivyo, katu hawakuwa na Mkutano endelevu na anayesema hivyo, afahamike kuwa anapotosha umma kwa maslahi yake binafsi kwa kuwa wanafunzi wasingeweza kupata majibu hayo kila mmoja akiwa nyumbani kwake.
2. Wanafunzi si sehemu ya mgogoro na wala katu, hawaungi mkono upande wowote wa mgogoro baina ya Menejimenti na Wahadhiri.
3. Wanafunzi kwa uwezo na nafasi yao, sio wataalamu wala waamuzi wanaoweza kuamua kama shughuli fulani ni mgomo au sio mgomo au basi kwamba, kama ni mgomo ni halali au sio mgomo halali. Hilo nalo wanafunzi hatujihusishi nalo kwa kuwa tunatambua kuwa sio kazi yetu.
4. Lengo kubwa hasa la safari yetu ya Dodoma lilikuwa jema tu, la kuiomba Serikali ifanye kila liwezekanalo kufungua Chuo mapema kwa kuwa wanafunzi tunateseka kwa kuahirisha mara kwa mara mihula (semester) ya masomo. Ikumbukwe kuwa, awali Chuo kilipaswa kumaliza Semester mwezi Julai na hata wahitimu kuhitimisha safari yao ya kitaaluma, lakini kipindi hicho kikasogezwa mbele hadi Septemba 2, 2011 ambayo pia inaonekana tena haitakuwa hivyo. Sisi ni tofauti na vyuo vingine ambavyo wanagomea masomo, lakini sisi tunalilia masomo.
5. Aidha, tulilenga kuieleza na kuionesha Serikali namna wanafunzi wanavyoishi maisha magumu kwa kuwa Mkataba wa Mkopo na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu ulishamalizika na pia, hata wenye nyumba yaani hosteli za nje, mkataba umemalizika na hivyo wanawatimua wanafunzi na kuwataka waingie mkataba mpya wa pango na kwa gharama mpya.
6. Mwisho, Kamati ililenga kuiomba Serikali kufanya uchunguzi, kubaini na hata kuondoa vyanzo vyote vya migogoro katika Taasisi hiyo kwa manufaa ya taifa letu.
MAPENDEKEZO YA KAMATI KWA WAZIRI WA AFYA
Ili kutowaathiri zaidi wanafunzi kwa mgogoro wasio husika nao, Kamati ilipendekeza kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kuwa, Serikali iingilie kati mgogoro uliopo baina ya Menejimenti na Wahadhiri ili sisi wanafunzi tusiendelee kuathirika.

MAJIBU YA MAWAZIRI
1. WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (DK. SHUKURU KAWAMBWA)
Alisema atakutana na Waziri mwenzake wa Afya na Ustawi wa Jamii (Dk. Mponda) kujadili na kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) na pia, akaahidi kulishughulikia ombi la wanafunzi kuwa Chuo kifunguliwe mapema ili wasizidi kuteseka kwa ugumu wa maisha na kuzidi kupoteza fursa mbalimbali zikiwamo za ajira kwa wahitimu. Aliwaomba wanafunzi kuwa wavumilivu na waendelee kujisomea wakati Serikali ikishughulikia matatizo yao mapema iwezekanavyo.
2. NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII (DK. LUCY NKYA)
Aliwahimiza Wanakamati waendelee kuwa watulivu kwa kuwa Serikali inashughulikia suala hilo.
3. WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII (DK. HADJI MPONDA)
Alisema tatizo linafahamika na Serikali inaguswa na matatizo ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii na hivyo, kuahidi kuyashughulikia haraka. Akijibu hoja ya Mheshimiwa Nchemba (MB) kuhusu usalama wa wanafunzi, Waziri Mponda alisema wanafunzi hao kwa vyovyote sio sehemu ya mgogoro , bali ni waathirika na hivyo Serikali iko makini kuhusu usalama wao ukiwamo wa kimasomo. Akizungumzia hoja ya Mheshimiwa Idd Azzan aliyeitaka serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wanafunzi namna ya kujikimu, Waziri Mponda alisema Serikali inaangalia namna ya kuwasaidia kwa muda utakaoongezeka.
HOJA ZA WABUNGE:
1. MHE. MWIGURU NCHEMBA –MBUNGE WA IRAMBA MAGHARIBI- CCM
Alimwambia Waziri Mponda katika mazungumzo hayo na Wanakamati kuwa, kwa kuwa mgomo haukuwa wa wanafunzi na wala hawakuwa sehemu ya mgogoro, Chuo kitakapofunguliwa ni vyema Serikali ihakikishe inasimamia wanafunzi wote warudishwe chuoni bila masharti wakiwamo Wanakamati wote yaani sisi.
2. MHE. IDD AZZAN – MBUNGE WA KINONDONI- CCM
Alimwambia Waziri Mponda (Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii) kuwa Serikali haina budi kushughulikia haraka kero zilizopo katika taasisi hiyo kwa wakati ili wanafunzi wamalize muhula wa masomo kwa wakati kwani wao sio sehemu ya mgogoro
TAMKO RASMI LA KAMATI
Kwa kauli hizo, Kamati inapenda kuutangazia umma wa Watanzania kuwa Serikali imeyapokea vizuri maombi ya Kamati hiyo na inawapongeza Waheshimiwa Mawaziri hao kutokana na ushirikiano na ukarimu waliouonesha kwa Kamati hii.
Pia, Kamati inawashukuru Mheshimiwa Mwiguru Nchemba (MB), Mheshimiwa Idd Azzan(MB) na Mheshimiwa Kassim Majaliwa; Mbunge wa Chalinze (CCM) kwa ushirikiano wao na ukarimu wao.

KATIKA HATUA NYINGINE,
Kamati imesikitishwa na taarifa iliyomnukuu Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Dodoma, Zelothe Steven ikisema wajumbe wanane wa Kamati hii (wanafunzi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii) wamekamatwa kwa tuhuma za kukutwa katika chumba kimoja katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Vatican mjini Dodoma.
Kamati inaamini kuwa Kamanda Zelothe alinukuliwa vibaya au hakueleweka vizuri na inapenda kuujulisha umma kuwa ilifika katika hiyo na kila mmoja alikuwa na chumba chake.
Asanteni

……………………………………………… …………………………………………………….. ………………………………………………
CHRISANT MUTATINA MARIAM SAAD KITAMOGWA, SAFARI
KAIMU M/KITI MAKAMU MWENYEKITI KATIBU
0717 745030 0717510851
0716760951 /
uni.Picha na Victor Makinda.

0716760951 / 0763432292

Post a Comment

Top