Menu
 

Imeelezwa kuwa huenda kuwa tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi katika viwanja vya maonesho ya kilimo nane nane mwaka huu likawa kubwa kuliko miaka iliyopita kutokana na mgao wa umeme unaendelea hivi sasa.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka jiji la Mbeya Injinia SIMIONI SHAURI wakati akijibu swali lililoulizwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya kuhusu suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi katika viwanja hivyo.

Awali katika swali lake la msingi mkuu wa mkoa wa Mbeya JOHN MWAKIPESILE alitaka kuelezwa namna ambavyo mamlaka ya maji safi imejipanga kutoa huduma ya maji safi katika kipindi chote cha maonesho.

Maonesho ya kilimo NANE NANE yanatarajia kufanyika kikanda mwaka huu mkoani Mbeya kuanza agosti mosi hadi nane mwaka huu katika viwanja vya JOHN MWAKANGALE vilivyo kata ya Isyesye jijini hapa yakiwa na kauli mbiu ya KILIMO KWANZA TUMETHUBUTU, TUMEWEZA na TUNAZIDI KUSONGAMBELE.

MGOMO BARIDI WA VIONGOZI MJI MDOGO WA TUNDUMA WILAYANI MBOZI.
Imedaiwa kuwa mji wa Tunduma wilaya Mpya ya Momba huenda ikakabiliwa na vurugu baada ya baadhi ya viongozi wa madereva wa magari ya mizigo kukubali kwenye mkutano jana kuendelea na kazi ya usafirishaji.

Habari zilizotufikia kwenye chumba chetu cha habari zinadai kuwa wasiwasi wa vurugu hizo umeanza kuonekana baada ya madereva wa magari makubwa kulazimishwa kuondoa magari katika kituo kikuu cha maroli cha Sogea -Tunduma na kuendelea na safari.

habari zaidi zinadai kuwa Madereva hao wanataka mgomo kuendelea na hivyo kuanza kuwashambulia viongozi wao  wakidai wamewasaliti baada ya kukubaliana na mkuu wa mkoa wa Mbeya kusitisha mgomo wao wakati Serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.

Mwenyekiti wa muda wa Madereva wa maroli yanayofanya safari zake nje ya nchi MOHAMED FIKIRI amesema msimamo wa chama chao ni kuendelea na mgomo nchi nzima.

  FOREST  JIJINI MBEYA. KAMATI YA NANE NANE
Hofu ya wamiliki wa vibanda vilivyopo pembezoni mwa uwanja wa nane nane Mbeya kuibiwa bidhaa zao imetajwa kuwa sababu ya wamiliki hao kushindwa kumalizia ujenzi wa vibanda vyao.

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya EVANSI BALAMA katika kikao cha kamati ya maonesho ya kilimo NANE NANE kilichowakutanisha wakuu wa mikoa mine ya kanda ya nyanda za juu kusini ambayo ni IRINGA, RUKWA, RUVUMA na MBEYA.

Pamoja na maelezo ya wamiliki wa vibanda hivyo mkuu wa wilaya amewataka kukamilisha ujenzi wa vibanda vyao kabla ya Serikali kufuta umiliki kwao na kuwapatia wengine.

Naye meya wa jiji la Mbeya ATANASI KAPUNGA amesema kuwa halmashauri haitoweza kuvumilia kuona uchafu wa majengo pembezo mwa barabara hivyo italazimika kuvunja endapo havitaendelezwa.

Mkutano wa leo umelenga kutatua changamoto zilizopo ndani ya uwanja wa maonesho ya kilimo nane nane ili kuwayafanya kuwa bora zaidi.
 

Post a Comment

 
Top