Menu
 

Kutokana na vurugu zinazoendelea Nchini Malawi mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile amesema Serikali mkoani hapa inaendelea na kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini humo ili kuwarejesha watanzania nyumbani.

Akiongea na Bomba Fm kwa njia ya simu Mwakipesile amesema taarifa za vurugu zimemfikia na kwamba hatua inayoendelea hivi sasa ni namna mbavyo watanzania wanaweza kurejeshwa nchini mwao wakiwa katika hali ya usalama.

Habari tulizo zipata hivi punde zinadai kuwa Wataalamu wa uchumi nchini Malawi wamesema kutokana na matukio ya maandamano nchini humo, serikali inapaswa kufikiria upya sera yake ya kushusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo.

Wasiwasi wa kiuchumi pamoja na kidemokrasia dhidi ya serikali ya rais Bingu Wa Mutharika huku kukiwa na upungufu mkubwa wa mafuta uliozusha ghasia nchi nzima siku ya Jumatano wakati waandamanaji walipotoa wito kwa Mutharika kujiuzulu.

Watu walipora maduka na kuchoma mali katika mapambano kati ya raia ya polisi nchini humo ambapo uporaji uliendelea katika baadhi ya maeneo ya Lilongwe na Blantaya jana Alhamis asubuhi na magari ya jeshi yameonekana yakifanya doria katika mitaa wakati jeshi liliitwa kuzima ghasia hizo.

MSIMU WA NANENANE NA MAANDALIZI YAKE MKOANI MBEYA.
Maonesho ya kilimo nane nane mwaka huu yatafanyika kikanda mkoani Mbeya na kuzinduliwa Agosti tatu na Waziri wa kilimo chakula na ushirika Profesa Jumanne Maghembe.

Akiongea na kamati ya maandalizi ya maonesho hayo mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile amesema kuwa maonesho yatafunguliwa Jumanne Maghembe na kufungwa agosti 8 na Waziri wa maji Profesa Marck Mwandosya.

Aidha amesema kila mkoa ndani ya kanda ya nyanda za juu kusini itakuwa na siku moja ya kusimamia shughuli za maonesho ambapo agosti 4 itakuwa kwa mkoa wa Mbeya, Agosti 5 mkoa wa Rukwa, Agosti 6 mkoa wa Iringa na Agosti 7 kwa mkoa wa Ruvuma.

Hata hivyo amewataka wananchi kutumia fursa ya maonesho hayo kuona shughuli zinazofanywa na wakulima kanda ya nyanda za juu kusini katika kusimamia na kutekeleza sera ya Kilimo kwanza.

Kauli mbiu ya maonesho ya kilimo Nane nane mwaka huu ni KILIMO KWANZA, TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE.

MAZINGIRA YABORESHWA SOKO LA IGAWAILO JIJINI MBEYA.
Hali ya usafi Mtaa wa Sokoni kata ya Igawilo imeendelea kuimarika kila siku Kutokana na juhudi ya kamati ya usafi wa mazingira ya mtaa huo kuhimiza wafanyabiashara na wananchi kutufanya usafi kwenye maeneo yanayowazunguka.

Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Alam Mbilinyi amesema baada ya kamati hiyo kuhamasisha umuhimu wa usafi wa mazingira na kuwatoza faini ya shilingi Elfu kumi kwa wale ambao maeneo yao ni machafu wananchi wa mtaa huo wamebadilika na kufuata utaratibu kwa kuzingatia kanuni za utunzaji wa mazingira.

Kutokana na hali hiyo Bwana Mbilinyi ametoa wito kwa wakazi wa mtaa wake kuendelea na tabia ya kufanya usafi katika maeneo yao ili kujikinga na hatari ya kupatwa na magonjwa ya milipuko.

BAADA YA BREAKING NEWS SASA NAKUJA NA HABARI KAMILI  YA MCHAWI KUKAMATWA.
Kijana mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake mkazi wa kata ya Nzovwe jijini Mbeya anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za ushirikina.

Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Forest ya zamani ambapo mtuhumiwa amekutwa akiwa juu ya nyumba za wananchi wa maeneo hilo.

Habari zaidi zinadai kuwa mtuhumiwa alikuwa akiruka juu ya paa za nyumba huku akikaa kwenye nyaya za umeme na kutoa lugha za vitisho dhidi ya vikosi vya usalama na wananchi ambapo pia kung’oa nyaya za umeme na antena.

Mwenyekiti wa mtaa wa Forest Bwana George Kazimoto amesema mtu huyo ametokea maeneo ya Nzovwe na kufika katika mtaa huo na kuruka katika nyumba ya Mama Tabitha na kuingia ndani na pale walipojaribu kumkamata jitihada hazikufanikiwa hadi pale lilipofika jeshi la polisi na kufanikiwa kumtia nguvuni.

Post a Comment

 
Top