Menu
 

Moja kati ya mabanda ya Maonesho yaliyowekwa katikka hali ya usafi
Mafundi rangi wakiwa kazini wakipaka rangi
Lango kuu la kuingilia uwanja wa Maonesho wa JOHN B MWAKANGALE Mkoani Mbeya

Maonesho ya kilimo ya Nane nane mwaka huu yatakuwa na mvuto wa aina yake kutokana na mpango madhubuti ulioandaliwa na muungano wa taasisi za wakulima Tanzania (TASO) kanda ya nyanda za juu kusini kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa kilimo.

Meneja wa maonesho hayo Bwana Kasilati Mwakibete amesema wadau wa kilimo kutoka mikoa ya Dar es saalam na Arusha wamekwisha wasili jijini Mbeya tayari kwa kushiriki maonesho hayo

Maonesho ya kilimo kada ya Nyanda za juu kusini yataanza agosti mosi hadi nane jijini Mbeya katika Viwanja vya John Mwakangale vilivyopo kata ya Isyesye na kufunguliwa agasti 03 na Waziri wa kilimo, chakula na Ushirika Profesa Jumanne Magembe na kufungwa agasti 08 na Waziri wa maji Profesa Marck Mwandosya.

HALI YA MIUNDOMBINU BADO NI TETE MBEYA VIJIJINI
Wakazi wa vitongoji vya DDC, Mtakuja na Mlima Reli wilaya ya Mbeya Vijijini wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 7 kutafuta huduma ya maji safi na salama.

Wakazi hao wamesema kutokana na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama wamekuwa wakilazimika kutumia maji ya Mto Mbalizi ambayo maji yake ni machafu na sio salama kwa matumizi ya binadamu.

Mmoja wa wanakijiji hao Michael Mwaifwani amesema licha ya kuwepo kwa miundombinu ya maji katika vitongoji hivyo bado upatikanaji wa huduma hiyo imekuwa ni tabu na kwamba wamekuwa wakilazimika kulipa bili ya maji ya shilingi elfu kumi kila mwezi.

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha DCC bwana Joined Mwalusanya amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa ongezeko la wakazi ni moja ya sababu inayopelekea utoaji wa huduma hiyo kusua sua.

Post a Comment

 
Top