Menu
 


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA ADVOCATE NYOMBI.
MBEYA RIPOTI YA MATUKIO
Matukio ya vifo, ubakaji na matumizi ya Dawa za kulevya mkoani Mbeya yameshuka kwa kiwango kikubwa kutokana na udhibiti unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoani hapa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ADVOCATE NYOMBI matukio ya ubakaji kuanzia mwezi Januari mpaka june mwaka 2010 ni 248 na mwezi januari hadi june mwaka 2011 ni 176 ambapo kati ya hayo kwa mwaka jana matukio 05 na matukio 03 kwa mwaka huu yametokana na unywaji wa pombe kupitia kiasi.

Aidha kwa upande wa Ajali za barabarani kwa kipindi cha mwezi januari hadi june mwaka 2010 kumetokea matukio 383 na kwa mwaka 2011 kuanzia mwezi januari hadi june ajali zimetokea 349 ambapo kati ya hizo ajali 8 kwa mwaka jana na 6 kwa mwaka huu zimesababishwa na ulevi.

Hata hivyo kwa mwaka jana matukio ya usalama barabarani yameonekana macheche zaidi kuliko mwaka huu ambapo mwaka jana makosa ya usalama barabarani yalikuwa 27,488 wakati kwa mwaka huu kuna jumla ya makosa 34160 hadi sasa.

MBEYA MAUAJI
Watu 6 wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti mkoani Mbeya likiwemo tukio la mwanafunzi mmoja wa darasa la sita wa shule ya msingi Itumbula kufariki dunia baada ya kupigwa viboko na mwalimu wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ADVOVATE NYOMBI mwanafunzi huyo ambaye amefahamika kwa jina la DANIEL KALISTO mwenye umri wa miaka 12 alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mbozi baada ya kuchapwa fimbo tatu na mwalimu wake aitwaye HAJI SIWILA ambaye amekamatwa na uchunguzi bado unaendelea

Tukio jingine limetokea kijiji cha Itumu wilaya ya Mbeya Vijijini ambapo mtoto TUMAINI SAIDI mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu amefariki dunia kwa kuungua na moto baada ya nyumba aliyokuwa amelazwa kuwaka moto kutokana na kibatari kuangukia kwenye godoro na kusababisha nyumba nzima kuwaka moto.

Aidha matukio mengine ya mauaji yamejitokeza wilaya ya Mbeya vijijini na Tunduma wilayani Momba ambapo watu watatu wamepigwa kisha kuchomwa moto na wananchi baada ya kuweka vizuizi barabarani kisha kuteka gari lenye namba za usajili T.851 AEK na kupora mali za abiria ambazo bado hazijafahamika na siku hiyo hiyo mtu mwingine ambaye anaye jina lake halijafahamika ameuawa na wananchi baada ya kukutwa akivunja Nyumba ya ANAD ERNEST na kuiba vitu vya thamani.

MBEYA MJINI
Chama cha Mapinduzi kesho kitafanya mkutano mkubwa na wa kihistoria jijini Mbeya katika viwanja vya shule ya msingi Ruanda Nzovwe vilivyopo kata ya Ilomba jijini Mbeya ambapo mkutano huo utaongozwa na viongozi wa chama hicho cha kitaifa.

Miongoni mwa viongozi watakao hutubia kesho  ni katibu wa halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi itikadi na uenezi NAPE NAUYE, Katibu wa Uchumi na Fedha MWIGURU NCHEMBA na mjumbe wa halmashauri ya kuu ya CCM taifa ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki SAMWELI SITA.

Wengine ni Mbunge wa jimbo la Peramio JENISTA MUHAGAMA, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro CHRISTOPHER OLE SENDEKA, Mbunge wa Same Mashariki ANNE KILANGO MALECHELA na Mbunge wa Singida LAZARO NYARANDU.

Habari kutoka ndani ya Chama hicho zinaeleza kuwa mkutano huo umelenga kutoa ufafanuzi kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya kuhusu dhana ya Chama Cha Mapinduzi ya Kujivua Gamba, kuhimarisha chama ikiwa ni pamoja na kueleza mafanikio yaliyofikiwa tangu Uhuru.

MBALIZI – MBEYA VIJIJINI
TUYAKE ZAMBI mwenye umri wa miaka 78 mkazi wa kitongoji cha Ijombe Iwindi amefariki dunia baada ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake wakati wakigombea Urithi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ADVOCATE NYOMBI amesema kutokana na tukio hilo Jeshi la polisi linamshikilia LACKSON ARISON mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni mjukuu wa marehemu aliyetaka kurithishwa mashamba kinguvu.

Kamanda NYOMBI amesema  TUYAKE ZAMBI alifikwa na mauti wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali teule ya Ifisi na kwamba upelelezi kuhusu tukio hilo bado unaendelea ili kubaini matatizo mengine yaliyomo kwenye familia hiyo.

KYELA
Zaidi ya Shilingi milioni mia moja arobaini na tisa, laki saba ishirini na mbili elfu mali ya kampuni ya BIOLEND Mikumi wilayani Kyela zimeporwa Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ADVOCETI NYOMBI amesema kuwa kufuatia tukio hilo Jeshi la polisi linawashikilia BWAKISA SENJELE mhasibu wa kampuni hiyo na RICHARD NYONI aliyekuwa akiendesha gari aina ya LANDCRUZA yenye namba za usajili T 149.AMH ambalo ndilo lililotumika kwenda kuchukulia fedha katika benki ya NMB Kyela.

Amesema kuwa majambazi waliopora fedha hizo walitumia silaha za moto na kumtishia dereva aliyebakia ndani ya gari hilo baada ya mhasibu kutelemka kilomita mbili toka ilipo benki hiyo.

Ameongeza kuwa tukio hilo limetokana na njama zilizopangwa kati ya watuhumiwa na majambazi hao na kwamba watuhumiwa wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

MBEYA

Viongozi wa dini wamehimizwa kujenga ushirikiano na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kudhibiti vitendo vya utoaji na upokeaji wa Rushwa mkoani Mbeya.

Wakiongea na viongozi wa Dini baadhi ya maofisa wa TAKUKURU mkoani hapa wamesema mafanikio ya mapambano dhidi ya Rushwa yanaweza kufanikiwa endapo viongozi watakuwa mstari wa Mbele kuwahubiria waumini wao kuhusu madhara ya utoaji na upokeaji wa Rushwa.

Maofisa wa dawati la Elimu kwa Umma la taasisi hiyo OMARY MTIMBO na ALLY NAKAPALA wamesema takwimu za ofisi yao hazioneshi mchango wa viongozi wa Dini katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Nao viongozi wa Dini walioshikiriki kwenye semina hiyo wamesema kuwa uelewa mdogo kati yao kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa ndio chanzo kikubwa kushindwa kushikiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Mkutano huo uliwashirikisha viongozi wa dini kutoka madhehebu ya dini ya kikristo na yele ya kiislamu.

CHUNYA
Raia wa wili wa Uingereza wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi mkoa kwa tuhuma za kukutwa na vipande vinne vya meno ya Tembo maeneo ya Mkwajuni wilayani Chunya mkoani Mbeya

Washitakiwa hao NICOLAUS VLADIMIRI na HOLLS CHAMBERS ambao wote wawili wamefikishwa mahakamani wiki lililopita na kusomewa  shitaka na Wakili GRIFFIN MWAKAPEJE  na hakimu mkazi ZABIBU MPANGULE.

Hata hivyo washitakiwa wote wawili walikana na kosa la kukutwa na nyara za serikali kinyume na sheria na kwamba wamerudishwa rumande mpaka pale kesi itakapo tajwa tena julai 21 mwaka huu.

Post a Comment

 
Top