Menu
 Mbunge wa Jimbo la Igunga Mkoani Tabora, Bwana ROSTAM AZIZ ametangaza kujivua gamba rasmi na kujiuzulu nyadhifa zote nakubakia na kadi ya CCM tu.

Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wazee wa jimbo lake la Igunga leo asubuhi, mbunge huyo amesema kaamua kuachia nafasi zake zote za uongozi ndani ya chama, akianzia ile ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa akiwa ni mjumbe toka Mkoa wa Tabora na ile ya ubunge.

Kwa mujibu ya mtandao wa JAMII FORUM, ROSTAM amesema uamuzi wake wa kuachia nafasi zake zote za uongozi alizopata kwa tiketi ya CCM haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ni kuachana na siasa hizo alizodai ni siasa uchwara (gutter politics) na amesema atatumia muda wake kushughulika na biashara zake.

 Aidha, amefikia uamuzi huo akiwa na lengo la  kuwajengea heshima na imani machoni mwa wanachama na wananchi wengine, viongozi wangu ambao anaamini baada ya yeye kujitoa watapata fursa ya kutafakari upya changamoto nyingine mbadala zinazowakabili ambazo msingi wake ni dhamana kubwa walizo nazo za kukiongoza chama na nchi kupitia Serikali yake.
 

Post a Comment

 
Top