Menu
 

 Mahakama ya mkoa wa Mbeya imetoa dhamana yenye masherti nafuu kwa Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini JOSEPH  MBILINYI pamoja na wenzake wawili wanaotumiwa kuandaa mkutano kinyume na taratibu.

Waliofikishwa mahakamani hapo ni pamoja na JOSEPH MBILINYI aka MR II/SUGU  Mbunge wa Mbeya Mjini, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya Mjini JOHN MWAMBIGIJA na Katibu Mwenezi wa CHADEMA Mkoa JOBU MWANYELELE ambao wamejidhamini kwa shilingi laki 3 na kesi hiyo itaendelea Septemba 6 mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge. Kwa mujibu wa katibu wa Mbunge FREDY MALIKI aka MKOLONI amesema Julai 8 mwaka huu na wenzake 7 wakiwa katika viwanja vya Nzovwe Sokoni walitiwa mbaroni na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuandaa mkutano kinyume cha taratibu za nchi.

Aidha amesema kutokana na taratibuanazozifahamu kwamba mbunge haombi kibali cha kufanya mikutano ya hadahara na badala yake hutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambao kazi yao ni kumlinda Mbunge asidhurike.

YALIOYOJILI BUNGENI 12 JULAI 2011
 UELEWA MDOGO WA WAKULIMA NDIO CHANZO CHA KUZULUMIWA RUZUKU ZA PEMBEJEO ZA KILIMO.


Uelewa mdogo wa wakulima juu ya matumizi ya ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa baadhi ya maeneo nchini imetajwa kuwa ni sababu kubwa ya kuzulumiwa pembejeo hizo na mawakala wa usambazaji.

Akijibu swali la GODFREY ZAMBI ambaye Mbunge wa Mbozi Mjini, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa JUMANNE MAGHEMBE ameyataja baadhi ya maeneo yaliyokuwa na undangayifu mkubwa na mawakala na viongozi wa kamati za pembejeo katika zoezi la usambazaji kuwa ni pamoja na Mioa ya Mbeya, Morogoro, Kigoma na Rukwa.

Amesema Mawakala 2335 kati ya mawakala 3,855 waliopewa mafunzo ya  usambazaji wa Ruzuku wa pembejeo za kilimo ndio wanaoendelea kufanya kazi nchini kutokana na kutimiza masharti ya kufikisha pembejeo kwa wakulima wasiokuwa na kipato chakutosha.

Amesema mawakala 1520 hawakutimiza masharti kutokana na kuwa na kesi mahakamani, kutokuwa na mitaji ya kutosha, udanganyifu na ufujaji wa pembejeo katika zoezi la usambazaji wa pembejeo kilimo, ambapo waefutiwa reseni..

Bwana MAGHEMBE ameongeza kuwa ametoa agizo kwa WAKUU WA MIKOA Nchini kufuatilia ni kiasi gani cha pembejeo kimepelekwa katika wilaya, tarafa, kata, vijiji na mkulima gani amepatiwa pembejeo, ili kuleta tija katika msimu wa kilimo ujao.UJENZI WA BARABARA KWA SASA NI KUUNGANISHA MAKAO MAKUU YA MIKOA.

Serikali imesema ipo katika zoezi la utengenezaji wa barabara zote zinazounganisha makao makuu ya mikoa kwa kiwango cha lami na baada ya kukamilisha mpaka mwaka wa 2017/2018, na kwamba baada ya kukamilika itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika vituo vyote vya huduma za jamii zikiwemo hospitali ili kurahisisha usafiri.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Dk HARRISON GEORGE MWAKIEMBE mbungni wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mtela Bwana LIVINGSTONE LUSINDE kuhusu ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Dodoma Mjini kuelekea hospitali ya Mvumi.

Amesema kuwa taifa ina-jumla ya kilometa 86,472 za mtandao wa barabara na kati ya hizo jumla ya kilometa 6, 318 za barabara ndizo zimejengwa kwa kiwango cha lami na kwamba, Barabara ya kuelekea hospitali ya Mvumi itaendelea kujengwa kwa kiwango cha Changarawe.  

Dk,. MWAKIEMBE amesema barabara zilizoanza kujengwa kwa lami katika kuunganisha makao makuu ya mikoani ni pamoja na Dodoma hadi Iringa, Singida hadi Tabora na Arusha hadi Manyara.

SABABU YA KUKATIKA KWA UMEME UWANJA WA TAIFA.

Naibu wa wizara ya Nishati na Madini Mheshimiwa BAKARI MALIMA amesema kuwa tatizo la kukatika kwa umeme katika Uwanja wa Taifa katika mechi ya Fainali ya Kombe la CASTLE KAGAME CUP 2011 baina ya YANGA na SIMBA, ilitokana na hitilafu ya umeme iliyotokea katika kituo cha Umeme cha KURASINI.

Amesema baada ya kugundua kuwa hitilafu hiyo imetokea katika laini ya umeme inayoelekea katika Uwanja huo, nakulazimika kurudisha katika maendeo mengine yasiyokuwa na hitilafu.

YANGA aliibuka na ushindi wa bao Moja liliofungwa na mcheaji ASSAMOAH katika dakika za nyongeza na kuifanya YANGA kuibuka na Kikombe hicho kwa Mara ya nne.

Post a Comment

 
Top