Menu
 

Gari alilokuwa akilitumia
 Marehemu Danny akiwa hospital

Mhariri wa gazeti la Rai, ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari, Danny Mwakiteleko, amefariki dunia.  

Habari ambazo blogu hii imezipata leo alfajiri na kuthibitishwa na watu wa karibu zinasema kwamba Mwakiteleko amefariki leo alfajiri katika hoispitali ya Muhimbili. Mwakiteleko alilazwa katika kitengo cha watu mahtuti Muhimbili baada ya ajali aliyoipata juzi usiku (jumatano) eneo la Tabata (ToT) na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala na baadaye Muhimbili. 

Katika ajali hiyo gari alilokuwa akiendesha Mwakiteleko liligongwa na lori lenye trela, ambalo lilitoweka bila kujulikana saa nne usiku. Mwakiteleko alikuwa akitokea kazini Sinza ambako alifanya kazi hadi saa tatu usiku. Mwakiteleko alipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa uangalizi hadi saa 12 asubuhi, ambapo madaktari waliamua apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili. 
                 Marehemu Danny enzi za uhai wake 
Baada ya uchunguzi Muhimbili, madaktari walisema majeruhi alikuwa ameumia kichwani na kumfanya apoteze fahamu kiasi hivyo ikabidi apelekwe katika chumba cha upasuaji ambako madaktari walimhangaikia kuanzia saa sita hadi saa tisa mchana.


"Bwana alitoa Bwana alitwaa

Jina la Bwana lihidimiwe"

Kwa hisani Kubwa na http://chingaone.blogspot.com/ 

Post a Comment

 
Top