Menu
 

CHUNYA MKOANI MBEYA.

Wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilayani Chunya Mkoani Mbeya wako hatarini kupoteza maisha kutokana na wazazi kuwapeleka watoto wenye ujauzito kwa waganga wa jadi ili kutoa mamba zao.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari kwa msaada wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umebaini kuwa vitendo hatari vimekuwa vikifanywa  kwa siri kubwa kati ya wazazi NA WAGANGA HAO WA JADI.

Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali teule ya Mwambani, wilayani hapo, Dakta BENANGODI KUSENGE amethibitisha kufanyika kwa vitendo hivyo ambapo tangu Mwaka jadi hadi mwaka huu wasichana watano wakiwemo wanafunzi Watatu walifariki dunia kutokana na vitendo vya utoaji Mimba kwa njia ya Kienyeji.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo MAURICE SAPANJO amesema tatizo la mamba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani humo limeendelea kutokana na wazazi kushindwa kutoa ushirikiano kwa serikali dhidi ya watu wasababishaji wa ujauzito kwa wananfunzi.

NZOVWE. JIJINI MBEYA.

Sakata la aliyekuwa Diwani wa Chadema , Kata ya Nzovwe jijini Mbeya , Bwana HEZRON MWAKALOBO, limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa kabla ya kuandika barua ya kujiuzuru, tayari, tayari alikabidhi kadi yake kwa katibu mkuu wa CCM mkoa , Bi VERENA SHUMBUSHO.

Mwakalobo alimkabidhi Katibu huyo kadi yake ya Chadema, yenye namba D.2009005150 Septemba 2 mwaka 2006.

Meya wa jiji la Mbeya, Bwana ATHANAS KAPUNGA WAKATI AKIZINGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI Mbeya amesema kuwa MWAKALOBO bado ni diwani halali wa kata hiyo na kuwa hajajiunga na Chama Cha Mapinduzi.

KAPUNGA amesema Julai 11, Mwaka huu , MWAKALOBO aliandika barua ya kujiuzuru nafasi hiyo aliyokuwa anaishikilia kwa tiketi ya CHADEMA, na kumkabidhi Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya.

Ameongeza kuwa taarifa za kujiuzuru kwa diwani MWAKALOBO, zimekwishafikishwa kwa katibu mkuu wa TAMISEMI na kwa Mkurungezi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).

Post a Comment

 
Top