Menu
 

Mwanamuziki Ludacris akizungumza jioni hii ndani ya Kempinsk hotel na Clouds TV,mara tu alipowasili jiji Dar..Ludacris ameahidi kukamua vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,litakalofanyika jumamosi hii ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Ludacris akijiweka sawa kwa ajili ya kurekodiwa na Wana Wa Clouds TV jioni ya leo.
Muwakilishi kutoka Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akiwafafanulia jambo Wageni aliokuja nao Mwanamuziki Ludacris jioni ya leo akitokea nchini Marekani.
Muwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akimuongoza Mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli aliyofikia -Kempinsk jioni ya leo mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onesho lake moja ndani ya viwanja vya Lidaz Club jijini Dar.
Muwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akisalimiana na kumkaribisha mwanamuziki Ludacris,mara kwenye hoteli ya Kempinsk mara tu baada ya kuwasili jioni ya leo akitokea nchini Marekani.
Mwanamuziki mahiri wa miondoko ya Hip Hop,ambaye pia ni muigizaji wa Filamu ajulikanae kwa jina la Christopher Bryian Bridges a.k.a Ludacris akiwasili leo jioni kwenye uwanja wa ndege wa Mwal Jk Nyerere na kupokelewa na Wenyeji wake.Mwanamuziki huyo ambaye ameletwa nchini na Kampuni Bingwa ya Burudani hapa nchini Prime Time Promotions Ltd/Clouds Media Group na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake maalum cha Fiesta 2011, Serengeti Primeum Lager

Post a Comment

 
Top