Menu
 

 Msanii Nicole Shwazinger Scherzinger memba wa kundi la Pussycat Dolls amekanusha taarifa zilizopo hivi sasa ya kwamba amechumbiwa na muendesha magari toka Uingereza, LEWIS HAMILTON


Nicole Scherzinger amekiri kuwa Uhusiano wao umedumu kwa miaka 4 sasa walipokuatana kwenye European Music Awards 2007,Munich-Ujerumani na kwamba, lakini hawana mpango wa kufunga ndoa kwa sasa.

Utata ulianza baada ya Baba yake Nicole kufunguka kwenye interview na kituo kimoja cha habari, alipoulizwa swali kuhusu mahusiano na kufunguka kuwa “mkwe wangu mtarajiwa ni mtu poa sana,familia nzima inamkubali”


BARNABA – DREAMS COMES TRUE KILA LA KHERI.
 
Zao la nyumba ya kukuza vipaji ya THT, BARNABA ndoto yake kumbwa ni kuhakikisha kwasasa anagonga kazi na Brazameni wa Kikongo man  Fally Ipupa ni baada ya mkongo man, kumfagilia Barnaba kwenye ukurasa wake wa Twiter kuwa anafurahishwa nae sana na kuahidi kuwa  ipo siku atafanya nae kazi.
 
 Barnaba alisema ilikuwa wafanye nae kazi siku nyingi, lakini kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kutoa wimbo wake wa 'Milele daima'ndio kilichomchelewesha.

  Kinda huyo kutoka THT alifafanua kuwa kama itawezekana kufanya kazi na mwanamuziki huyo mkongwe Barani Afrika itakuwa ni nafasi nyingine kwake kuonyesha uwezo wake kimataifa baada ya kuonyesha kipaji chake hapa nyumbani.


LICHA YA KUWA  NA MADENI MANCHESTER UTD YAONGOZA KWA UTAJIRI.
Timu ya Manchester United ya England aka The Red Devils,imetajwa na jarida la Forbes aka Forbes magazine kuwa ni the most valuable sports team in the world kwa mwaka wa 3 mfululizo pamoja na deni linalofikia paundi milioni 475 
                 
Timu za Real Madrid na Arsenal ni timu pekee zinazotoka bara la ulaya zilizomo kwenye top 10....

1 Manchester United £1.165billion
2 Dallas Cowboys £1.13bn
3 New York Yankees £1.06bn
4 Washington Redskins £960million
5 Real Madrid £900m
6 New England Patriots £850m
7 Arsenal £740m
8 New York Giants £734m
9 Houston Texans £727m
10 New York  Jets £708m

Post a Comment

 
Top