Menu
 

 Mjengo atakaofilisiwa jamaa

Nguli wa muziki wa R&B duniani na mshindi kibao za gramy,bet mtv na zingine kibao r-kelly ataweza kufilisiwa baadhi ya mali zake. kama R. Kelly  anakumbuka mistari ya kibao chake cha  "Trapped in the Closet," lazima atakuwa anajiamini na kusahau kulipa deni hilo kwa mujib wa uamuzi wa mahakama mwezi uliopita ktk jimbo la chicago, the R&B singer (born Robert Kelly) alitakiwa kulipa deni hilo toka mwaka 2010 june alikopa11 years ago. amelipa $2.9 million na kudaiwa zaidi ya $3.5 million pamoja na riba  toka mwaka 1999.

        Jamaa amekuwa kwenye matatizo kwa muda  mrefu tangu mwaka 1996 ambapo alishitakiwa kwa kuwa kwenye mahusiano na Serengeti girl yan msichana mwenye umri chini ya 18 na mwaka 22 alishitakiwa tena kwa kufanya kosa lilelile la kulala na mwanamke wa chini ya umri
       
Mwaka 2006 ne-yo alimshitaki r Kelly na kutaka alipwe $ 700,000 na mwezi mmoja baadaye jamaa alivunja mkataba na manager wake na kutakiwa kulipa $1 million kwa kuvunja mkataba.

Hata ivo R KELLY ni miongoni mwa wanamziki watakao perfom ktk uzinduzi wa kituo kikubwa cha iHeartRadio Music Festival litakalofanyika 23-24 mwezi wa tisa  las vegas wengine ni.Lady Gaga, Coldplay, Bruno Mars and Nicki Minaj Alicia Keys, Rascal Flatts and the Black Eyed Peas, are among a slew of performers who will swarm on Las Vegas in  , Ryan Seacrest alitangaza jumatatu Seacrest atakuwa mc wa tamasha hilo


ILOMBA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, SAMUEL SITTA, ametaka kuanzishwa kwa mjadala ndani ya Serikali wa kuwaadhibu viongozi waliolisababishia Taifa mgawo wa umeme ambao amedai kuwa unaifedhehesha nchi.

Waziri SITTA amesema miradi ya umeme ikitekelezwa kwa uadilifu nchini, Tanzania ina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kwa matumizi yake na ziada kuuzwa katika nchi jirani zilizo Kaskazini na Kusini mwa bara la Afrika.

Amesema ukiwa serikalini vinakuwepo visingizio vingi, lakini katika suala la umeme lazima turekebishane kwani nchi hii sio ya kuwa na mgawo wa umeme bali ni nchi ambayo inastahili kuwa na umeme wa kutosha na mwingine kuuza nje.

Sitta ameyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye kongamano la vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Vyuo Vikuu vilivyopo mkoani Mbeya, liliwashirikisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Dakta HARRISON MWAKYEMBE, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, LAZARO NYARANDU, Mbunge wa Mbozi Mashariki, GODFREY ZAMBI, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), MARY MWANJELWA, Mbunge wa Simajiro, CHRISTOPHER OLE SENDEKA .

MBEYA
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Bwana NAPE NNAUYE amesema dhana ya kujivua gamba si yake bali ni ya Chama baada ya kuona kwamba kimepoteza mwelekeo.

Kauli hiyo aliitoa jijini Mbeya katika mkutano wa hadhara wa viongozi wa kitaifa wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Ruanda Nzovwe ukiwa na lengo la kuwafafanulia wananchi juu ya dhana ya CCM kujivua gamba.

Amesema katika mkutano huo kwamba kilichotokea mpaka chama kikapoteza mwelekeo ni sawa na wauza duka waliotumwa ambao waliamua kujipangia bei zao wao wenyewe.

Kauli ya NAPE inaonekana kumjibu aliyekuwa Mbunge wa Igunga, ROSTAM AZIZ ambaye katika hotuba yake ya kujiuzulu nyadhifa zake katika CCM aliwashambulia Nape na Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara JOHN CHILIGATI na kusema wamepotosha dhana ya kujivua gamba na kuanza kuwasakama wanachama watatu wa CCM akiwamo Rostam kwa tuhuma za ufisadi.

Mkutano wa CCM mkoani hapa ulihudhuriwa na maelfu ya watu, hali kadharika wananchi wapatao 2689 wajiunga ccm wakiwemo 400 kutoka vyama pinzani

Post a Comment

 
Top