Menu
 

 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, amewataka Watanzania kutoa elimu kwa vijana juu ya umuhimu wa kuwepo kwa wazee ili kuepukana na mauaji ya vikongwe ambayo yamekuwa yakifanyika zaidi katika Kanda ya Ziwa.

Amesema serikali haina mkakati wowote mbali ya jamii kuhamasishwa kutoa elimu kwa vijana ili kuweza kutambua mabadiliko ya viungo vya mwili pindi unapokaribia umri wa miaka 45  uwezo wake wa kimwili hubadilika ambapo macho kuwa mekundu, masikio pamoja na viungo vingine vya mwili hupoteza asili yake ya mwanzo.

Nahodha amesema kati ya mwaka 2005 hadi mwaka jana matukio ya mauaji ya vikongwe yaliyoripotiwa nchi nzima ni 2,575 na jumla ya watuhumiwa 2,183 walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo.

Hata hivyo watuhumiwa waliokamatwa 1599 walifikishwa mahakamani na baadhi yao kesi zao zimekwisha na wengine kesi zao zinaendelea kusikilizwa na nyingine ziko katika hatua nzuri.

VIONGOZI WAKUTANA ROMA JUU YA JANGA LA NJAA AFRIKA


Shirika la Umoja wa Mataifa la  Mpango wa Chakula Duniani leo litaanza kusafirisha kwa ndege misaada ya vyakula hadi Somalia.

 Mkuu wa shirika hilo, Josette Sheeran, alitoa tangazo hilo katika mkutano wa dharura uliofanywa Roma kuzungumzia namna jamii ya kimataifa itakavokabiliana na ukame ulioko katika Pembe ya Afrika.

Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO, Bwana Jacques Diouf, aliufungua mkutano huo akito mwito kuchukuliwe hatua:

"Tunabidi tunusuru maisha na kuokoa maisha na kulipatia jibu hali hii ya dharura ili kuepusha kuzidi hali kuwa mbaya. Madhara yanayotokana na ukame, ughali wa maisha na migogoro yamezusha hali ya kutisha inayolazimisha papatikane msaada mkubwa wa kimatifa na wa haraka."

Ukame huo mbaya kabisa kuwahi kuonekana katika eneo hilo tangu kupiti miaka sitini sasa umesababishwa watu milioni 12 wawe katika ukingo wa kufa kwa njaa. Benki Kuu ya Dunia imeahidi kutoa Euro milioni 350 kwa ajili ya miradi ya kilimo ya muda mrefu ili kulisaidia eneo hilo.

Post a Comment

 
Top