Menu
 

 
T-PAIN anatarajia kutengeneza MIC itakayokuwa inaitwa I am a T-PAIN MIC ambazo zitawawezesha watoto  kuzisikia sauti zao zikiwa na sound effects (auto tune).

Pia kuna tetesi jamaa kutoa ngoma nyingine itayokuwa na kiwango cha juu cha auto tune kwa teknolojia ya juu kutoka katika studio anayomiliki kwenyewe.

Karne tatu zilizopita kuna jamaa anayeitwa JAKKS PACIFIC alikuwa anatumia kibox kilichokuwa kinatumia umeme, kilichofanya sauti yake itoke na auto tune.

The I Am T-Pain Mic zinakuja kwa rangi tatu tofauti, rangi ya nyeusi, dhahabu na nyeupe hivyo watoto kaeni mkao wa kula.
LADY GAGA, MINAJI, MARS NDANI YA SHOW MOJA.

 
Mkali wa miondoko ya POP, LADY GAGA ni Mwanadada ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwa vituko.Hivi karibuni hajaishiwa vituko baada ya kutinga Club na vazi lenye material ya Pazia.
 
NIKI MINAJ toka YONG MONEY CASH MONEY BROTHERS (YMCMB)
Lady Gaga, Coldplay, Bruno Mars na Nick Minaji ni miongono mwa watu watakao pafom ktk tamasha kubwa litakalo fanyika LAS  VEGAS sept mwaka huu litakalo itwa  ‘heart radio music festival’. Habari hizo zimetolewa na Ryan Seacrest..

Ryan ndiye atakaye sherehesha shughuli hiyo iliyo andaliwa na kituo kikubwa cha radio marekani.

Pamoja na kuwa sherehe hizo zita shereheshwa na mshereheshaji maarufu Ryan,pia kutakuwa na wana muziki wakongwe na walio weza kukonga nyonyo za watu kipindi cha nyuma toka America kama, Jenifa Lopez, Carrie underwood na Kelly Clarkson.

KUMBUKUMBU ZA KUZALIWA LEO.

 GERALD R. FORD Amezaliwa 14 - Jul – 1913, angetimiza Umri wa miaka 98 kama angekuwa hai.
Rais wa awamu ya 38  nchini MAREKANI kuanzia mwaka 1974 – 1977

SUSANA MARTINEZ Amezaliwa 14 - Jul – 1959 anatimiza umri wa miaka 52.
Gavana wa kwanza mwanamke mwenye asili ya kilatini nchini MAREKANI ambaye ni raia wa MEXICO
Imeandikwa na Chris Bee na Tonny Thebest.

Post a Comment

 
Top