Menu
 

Tunapenda kulitambulisha watanzania wote waishio popote Duniani kwamba kuanzia sasa wanaweza sikiliza Radio kupitia mtandao yani Internet Buree. Tumeona tufanye hivi kwa kutambua kwamba pamoja na kuwa watanzania wengi wapo hapa nchini na wengi wao kwa sasa wanatumia mtandao na wanapenda sikiliza Radio kupitia mtandao, lakini pia tumezingatia na watanzania wenzetu wanaoishi nje ya nchi wapate Burudani, Habari na mambo mengine mengi kutoka Tanzania. Kupitia Tone  Internet Radio watakuwa hawajisikii upweke na kuona kama wapo Tanzania. Pia Tone Radio inawapa wasanii wa Muziki wa aina yoyote Tanzania kuleta nyimbo zao hapa studio na sisi kutangaza kazi zao bure kwa kututumia nyimbo zao kupitia toneinternetradio@yahoo.com .

Bofya hapa kusikiliza Live: http://www.toneinternetradio.blogspot.com 


Tunatanguliza Shukurani Zetu za Dhati na karibuni sana... Tone Internet Radio Pamoja Tutafika

Fredy Anthony Njeje
Chief Multimedia Architect
Tone Multimedia Company Limited 

WATATU WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO MBEYA VIJIJINIWatu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa na  wananchi wenye hasira  na kisha miili yao kuchomwa moto wakiwa wanajaribu kuteka gari la abiria kwenye eneo la Igoma  lililopo Mbeya Vijijini.

 Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, amesema tukio hilo lilitokea Julai 14 mwaka huu majira ya saa tano za usiku  katika  msitu wa hifadhi ya Taifa Ilenga kijiji cha Igoma. Amesema, majambazi hao wanadaiwa waliweka vizuizi kwenye barabara ya Igoma/ Kikondo  na kisha kuteka gari lenye namba za usajili T.851 AEK ISUZU  Lori lililokuwa limebeba mizigo.

 Amesema kuwa gari hilo likiwa limebeba mizigo pamoja na abiria   ambapo majambazi hao walisimamisha gari hilo na kufanikiwa kupora badhi ya vitu na simu . Amesema, wakiwa wanafanya tukio hilo baadhi ya wakazi wa eneo hilo walipata taarifa na ndipo walipoamua kufanya msako na kufanikiwa kuwakamata majambazi hao na kuanza kuwapa kichapo na kisha kuwachoma moto.

 Nyombi, amefafanua kuwa  askari walifika eneo la tukio na kukuta watu hao wakiwa wemeteketea kwa moto na kwamba , kamanda amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Post a Comment

 
Top