Menu
 

 Uwanja wa Ndege Mkoani Mbeya Tanzania
Uongozi wa uwanja wa ndege Mbeya umesema kuwa mwananchi atakaye kamatwa akikatisha kwenye uwanja wa ndege huo atatozwa faini ya shilingi elfu 30 ili kuepusha hatari ya kutokea maafa wakati wa ndege kutua na kuruka.

Kiongozi wa ulinzi wa uwanja huo Bwana Peter Mbugi amesema kuwa adhabu hiyo imewekwa ili kuimarisha usalama wa usafiri wa anga ambao umekuwa ukikabiliwa na tatizo la wananchi kukatisha uwanja hapo.

Wakazi wa mtaa wa Air Port, Iyela, Isengo na Hali ya Hewa wamekuwa wakikatisha kwenye uwanja huo ili kupunguza umbali wa safari zao wakati wa kufuata mahitaji muhimu sehemu mbalimbali za jiji.

Post a Comment

 
Top