Menu
 

 Soko dogo la Uyole Jijini Mbeya Tanzania
 Mchele akiwa umeshakobolewa tayario kwa Matumizi ya Chakula na Biashara katika Masoko.
Mpunga ukiwa bado haujakobolewa kuwa mchele.

Bei ya mchele soko la Uyole imepanda kutoka shilingi elfu ishirini na moja mia tano hadi kufikia shilingi elfu ishini na tano kwa debe kutokana na kupanda kwa gaharama za usafirishaji.

Mmoja wa wafanyabiashara wa mchele sokoni hapo Bi.Huruma Jacob amesema licha ya kupanda kwa gharama za usafirishaji pia upatikanaji wa mpunga umekuwa mdogo kutoka kwa wakulima.

Kwa mwaka huu, hali ya kilimo cha mpunga mkoani Mbeya haikuwa nzuri kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yaliyoikumba nchi yetu mwanzoni mwa mwaka huu.

Post a Comment

 
Top