Menu
 

Hatimaye Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekamilisha mchakato wa kuwapata wagombea wake wa viti vya udiwani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Kata ya NZOVWE na MAJENGO jijini MBEYA.

Akizungumza na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini Bwana Christopher Mwamusiku amesema Mchungaji David Mwashilindi ndiye atakayewania kiti cha udiwani Kata ya NZOVWE na amemtaja Bwana Joseph Mwasampeta kugombea nafasi hiyo kwa kata ya MAJENGO.

Ameongeza kuwa wao CHADEMA wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi katika Kata zote mbili dhidi ya vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo.

Kampeni zitaanza tarehe kumi mwezi ujao kwa vyama vitakavyoshiriki uchaguzi na tarehe mbili Oktoba mwaka huu ndiyo itakuwa siku ya Uchaguzi.

Post a Comment

 
Top