Menu
 

Aliyekuwa Kaimu Kamishna wa wa polisi mkoa wa Dar es Salaam, Abdalah Zombe, akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama kuu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Picha na Victor Makinda

Katika maelezo yake Zombe alisema kuwa anamshangaa Mbunge wa Arusha mjini,ambaye pia ni Waziri Kivuri wa Mambo ya Ndani Godbles Lema, kwa kitendo chake cha kuhoji kuhusu uhalali wa hukumu ya Zombe katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge. Zombe alisema kuwa Lema, hajui katiba ya Tanzania. Akifafanua alisema kuwa Lema kama mbunge/Bunge ni muhimili wa Dola unaojitegemea. Mahakama pia ni muhimili wa Dola unaojitegemea. Hivyo alishangaa kitendo cha Lema (MB) kuhoji maamuzi halali ya Mahakama.
Akiongeza alisema kuwa Wbunge wa CHADEMA hawajui watendalo bungeni na aliapa kuwa endapo Chadema watapata ridhaa ya kuongoza nchi, yeye Zombe atajinyonga. 'Endapo kama CHADEMA watatawala nchi hii, mimi nitajinyonga kabisa' Hiki ni chama cha hovyo na wabunge wake ni wa hovyo. Hawaijui katiba,alisema.


Post a Comment

 
Top