Menu
 

Chama cha waendesha pikipiki mji mdogo wa Mbalizi kimeomba Serikali kuweka sheria itakayombana abiria kuvaa kofia pindi anapopanda pikipiki badala ya sheria hiyo kumbana deriva pekee.

Wamesema polisi wa usalama barabarani wamekuwa wakiwatoza faini maderera pekee pindi wanapokamatwa kwa kosa la abiria kuto vaa kofia wakati kosa hilo husababishwa na abiria mwenyewe

Makamu mwenyekiti wa waendesha pikipiki Mbalizi bwana Festo Lwesha amesema baadhi ya abiria wamekuwa wakikataa kuvaa kofia wanapokuwa wamepanda pikipiki kwa kuhofia kupatwa na magonjwa ya ngozi kupitia kofia hizo.

Mmoja wa abiria ambao wanahofu ya kupatwa na magonjwa ya ngozi kupitia kofia za pikipiki mkazi wa Utengule Bi.Jacklin Mwangela amesema wanakataa kuvaa kufia hizo kwa sababu ni chafu na zinanuka na kuna uwezekano mkubwa wa kuambukizana magonjwa ya ngozi.

Naye mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mbeya Ezekel Mgheni amewataka maderera wa pikipiki kuwavisha wateja wao rambo kabla ya kuwavisha kofia ili kuwaondolea hofu ya kupatwa na magonjwa ya ngozi kupitia kofia hizo na kuongeza kuwa sheria inabidi iangaliwe upya ili abiria nao waweze kubanwa.

Post a Comment

 
Top