Menu
 

Watoto wadogo raia wa kigeni ambao wazazi wao watakamatwa kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wataanza kuwa chini ya uangalizi wa kituo cha kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi hadi hapo wazazi wao watakapomaliza kutumikia adhabu yao.

Hayo yameelezwa na mkuu wa kituo cha CHILD SUPPORT TANZANIA bwana Omoding James mara baada ya kupokea msaada kutoka shirika lisilo la kiserikali la INTERNATIONAL ORGANIZATION FOR MIGRATION ili kukiongezea kituo hicho uwezo wa kutoa huduma kwa watoto wadogo.

Amesema kituo kimepokea vitanda kumi dabodeka kwa ajili ya kusaidia kuboresha huduma za malazi kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na wale ambao wazazi wao watakuwa wakitumikia kifungo kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.

Naye afisa polisi jamii Inspekta Majaliwa amepongeza hatua za mashirika hayo katika kutoa huduma bora kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wa ndani na nje ya nchi na kuongeza kuwa mpango huo utaongeza ushirikiano kati ya Tanzania na nchi jirani.

Post a Comment

 
Top