Menu
 

 Papai ni tunda moja lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha.

Tunda hili huepusha maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu. Kinga dhidi ya magonjwa ya moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.

Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu, na ule unaotokana na kupatwa na kisukari. Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.

SIGARA HUATHIRI MAPAFU KIVIPI NA INAKUAJE?.
 Kama wewe ni mvutaji wa sigara kupita kiasi/mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.

 UGONJWA WA SARATANI KATIKA KIBOFU.
Wataalamu hushauri kutumia matunda kwani ni moja kati ya tiba ya magonjwa madogo madogo na hatarishi hivyo basi Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo.

Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.

Post a Comment

 
Top