Menu
 HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHE. MCHUNGAJI PETER MSIGWA, (MB) WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA 2011/2012.
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Kambi rasmi ya Upinzani,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Kambi yetu kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2011/2012, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99(3) na (7) toleo la 2007.
Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kumsifu, kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwenye nguvu na hekima tele kwa kunipa afya njema na kuendelea kunipigania kwenye kila jambo. Kama alivyomuwezesha Daudi kuibuka mshindi dhidi ya Goliath, jitu kubwa na lenye nguvu nyingi, ndivyo alivyoniwezesha mimi kushinda uchaguzi na kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini. Kwa makusudi yake maalum, ambayo sina budi kuyatekeleza nikifuata uongozi wake, namshukuru kwa kunifanya sehemu ya Bunge hili la Kumi, ambalo binafsi naamini ni Bunge la Kimapinduzi.
Mheshimiwa Spika, kwa nafasi ya kipekee kabisa, namshukuru mke wangu mpenzi, Mama Kisa Msigwa, watoto wetu Jimmy, Peter Junior, Semione, Karren na mapacha wetu, Jacqueline na Jocelyn, kwa upendo na sala zao kwangu. Na huko waliko nawaomba wakumbuke kuwa; “The value of our dignity in this World will never be determined by what we have accumulated, but rather for what we have contributed. Thamani ya utu wetu hapa duniani haitatokana na.... Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com

Post a Comment

 
Top