Menu
 

Kufuatia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan biashara ya viazi vitamu,ndizi,magimbi,mihogo,tende na tambi katika soko la Sokomatola jijini Mbeya,vimekuwa na soko kubwa kwa mahitaji ya Waisilamu ambao hununua kwa ajili ya Futari na Daku.

Mmoja kati ya wanunuzi wa vyakula katika soko hilo Bi. AMINA RAMADHANI amesema kwamba inamlazimu kununua vyakula hivyo kutokana na mahitaji ya mwezi huu ambao vyakula mahsusi vya Futari na Daku huhitajika.

Mmoja wa wauzaji katika soko hilo Bwana MUSA ALLY ameeleza kuwa uuzaji wa vyakula hivyo unamuingizia kipato kikubwa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Post a Comment

 
Top