Menu
 

Idadi kubwa ya wanawake wamejitokeza kupima virusi vya ukimwi ndani ya viwanja vya John Mwakangale kwenye maonyesho ya nanenane jijini Mbeya yalioanza tarehe mosi Agosti mwaka huu.Hayo yamesemwa na mmoja wa washauri wa kituo cha kupima na kutoa ushauri nasaha Kihumbe Bi.Eva Lutangilo kuwa wananchi wameonyesha mwamko mzuri kutaka kujua afya zao wakiongoza wanawake.Ameongeza kwamba licha ya upimaji wanatoa elimu juu ya virusi ukimwi jinsi unavyoambukizwa, dalili zake na jinsi ya kujikinga dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na ngono.

WANAFUNZI WAJISHUGHULISHA NANE NANE NYAKATI ZA MASOMO. 

Baadhi ya Wanafunzi wa shule za msingi jijini Mbeya wameonekana wakijishughulisha na kazi mbalimbali katika uwanja wa maonesho ya kilimo Nane nane badala ya kuwa masomoni.

Watoto hao wamekuwa wakijishughulisha na shughuli za usafi wa mabanda, michezo ya kamali na kubeba mizigo ya baadhi ya wafanyabishara ndogondogo uwanjani humo.

Watoto hao wamekuwa wakionekana kwenye viwanja hivyo muda ambao ni wa masomo huku wakiwa wamevalia sare za shule.

Mtoto Shoham James mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Gombe iliyopo kata ya Uyole amesema ugumu wa maisha na kipato duni cha familia ndio sababu inayowafanya kushindwa kuwa masomoni muda wa masomo na badala yake wanajishughulisha na kazi mbalimbali kwenye maonesho hayo ili waweze kujipatia kipato.
 

Post a Comment

 
Top