Menu
 

                                Bustani nzuri Jijini Mbeya
                   Stendi ya Kwambe Mwanjela Jijini Mbeya.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mbeya Ezekiel Mgeni ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapowaona madereva wakikatisha safari zao na kuongeza kuwa kitendo hicho kinyume na taratibu za usafirishaji

Ombi hilo limetolewa na Kamanda MgeniI ambapo ameongeza kuwa kitendo hicho husababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wawapo safarini.

Nao baadhi ya wakazi wa kata za Isyesye, Uyole na Igawilo ambao ni waathirika wakubwa wa tatizo la madereva kukatisha safari zao wamesema kitendo hicho kimekuwa kero kubwa kwao na kuahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa Jeshi la polisi ili kudhibiti vitendo hivyo.

Aidha miongoni mwa wakazi hao Fatuma Abubakar, Dominic Tuntufye na John Luvanda wameiomba jamii kuwa na ushirikiano ili kuweza kudhibiti tabia ya madereva kukatisha safari zao kwani kitendo cha abiria kukubali maamuzi ya madereva na makonda ndicho kimechangia tabia hiyo kuwa Sugu.

Post a Comment

 
Top