Menu
 

Jeshi la polisi mkoani Mbeya limeanza kufanya upelelezi wa wezi na vibaka ambao wamekuwa wakivunja milango na Kuiba pesa na vitu vya samani kama deki, computer na laptop katika katika maeneo mbalimbali jijini Mbeya.

Msemaji wa jeshi la polisi Mkoani Mbeya Inspector Majaliwa amesema kuwa wamepokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa kata ya Iyela kuhusu kuwepo kwa vibaka na wezi wanaovunja milango kisha Kumba wakati wenye mali hawapo.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Block T. Bwana Adrian Majembe amesema kuwa mbinu wanayotumia wezi hao ni kuluka ukuta na kuvunja makufuli ya nyumba kisha kuingia ndani na kuiba.

Aidha amewaomba wananchi wa mitaa ya Block T, Isengo, Pambogo na Nyibuka kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi linapohitaji taarifa ya wahalifu kwenye makazi yao ili kudhibiti vitendo hivyo.

Post a Comment

 
Top