Menu
 

Baadhi ya wapangaji wa vyumba vya biashara jijini Mbeya ambao shughuli zao hutegema kuwepo kwa umeme wamewalalamikia wamiliki wa vyumba hivyo kwa kuendelea kuwatoza kodi ileile na baadhi ya kuongeza liicha ya mgao mkali wa umeme unaoendelea nchini kote.

Wakiongea kwa nyakati tofauti kwa sharti la kutotaka kutajwa majina yao wamesema mgao wa umeme umekuwa ukichangia kupatikana kwa mapato kidogo na wakati mwingine hulazimika kufunga sehemu zao za kazi hali inayosababisha kutolipa kodi kwa wakati muafaka na ugumu wa maisha.

Aidha wamewaomba wamiliki hao kuwa na subira wanapodai kodi zao na kutopandisha kodi mara kwa mara maana hali hiyo inawaathiri sana kiuchumi kwani uhaba wa nishati ya umeme ni suala linalojulikana.

Kwa upande wao baadhi ya wamiliki wamesema kuwa na wao ni miongoni mwa wanaokabiliwa na tatizo hilohilo kwani nao wana shughuli zinazotegemea kuwepo kwa umeme na kwamba kilio chao ni kimoja na wanategemea serikali kuwa mfariji wao.

Post a Comment

 
Top