Menu
 

Uchumi wa wafanyabiashara wa maduka ya vifaa vya kitaaluma (stationary) umeyumba kutokana na tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme linaloendelea hapa nchini.

Akiongea na Chimbuko Letu mmoja wa wafanyabiashara hao Bi.Frida Msuya amesema kutokana na mgao mkali wa umeme unaoendelea wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao hali inayopelea kukosa fedha kwa ajili ya kulipia pango la biashara.

Aidha ameuomba uongozi wa shirika la umeme mkoani Mbeya kuwa na usawa kwa ugawani wa nishati hiyo ili kuwawezesha wananchi kuipata nishati hiyo kikamilifu.

Kwa mkoa wa Mbeya imekuwa ni jambo la kawaida kwa maeneo ya Forest, Iyela, Ilemi, Ilomba, Uyole, Isyesye, Itezi, Mwakibete, Igawilo na Mbalizi kukosa umeme kwa zaidi ya siku moja.

Post a Comment

 
Top