Menu
 

Maandamano yaliyopangwa kufanywa na wakazi wa eneo la Bomba Mbili kata ya Mwakibete yamesitishwa baada ya uongozi wa Serikali ya mtaa kwa kushirikiana na mwandishi wa habari kutoka Bomba Fm kutoa ufafanuzi kuhusu tatizo la maji jijini hapa.

Wakiongea kwenye mkutano wa dharula wawakilishi hao wa wananchi wamesema tatizo la maji limechangiwa kwa kiasi kikubwa na mgao wa umeme unaendelea hapa nchini.

Awali balozi wa mtaa huo Daimon Mwanjali kwa kushirikiana na mwandishi wa habari wa Bomba Fm walikwenda hadi ofisi ya idara ya maji kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu tatizo hilo na baada ya kufika walitembezwa kwenye vyanzo vya maji na matenki ambapo walishuhudia kutokuwepo kwa maji kwenye matenki kutokana na mitambo inayotumia umeme kushindwa kusukuma maji kwenda kwa wananchi.

Aidha katika mkutano huo wakazi wa Mwakibete wameiomba idara ya maji kutoa bili ya maji kulingana na matumizi ya mteja.

Post a Comment

 
Top