Menu
 

Mamlaka ya udhibiti wa nchi kavu na majini SUMATRA jijini Mbeya imewataka wamiliki wa daladala, madereva na makondakta kuhakikisha wanatoa tiketi kwa abiria ili kuthibitisha nauli halisi anayotakiwa kutoa abiria.

Hayo yamesemwa na afisa wa Sumatra mkoa wa Mbeya Amani Shamaje wakati wa mahojiano kuhusu hatua inayochukuliwa na mamlaka hiyo kuthibiti vitendo vya upandishwaji wa nauli kiholela.

Amesema bei halali ya daladala kutoka majengo, sokomatola hadi sai ni shilingi mia tatu na uyole ni shilingi mia tatu hamsini na kwamba kutoka mwanjelwa, soko matola hadi iyunga ni shilingi mia tatu wakati kutoka sokomatola, mwanjelwa hadi mbalizi ni shilingi mia tatu hamsini.

Wakati huohuo amewataka makondakta na madereva kuvaa sare vizuri na kuzifua ili kuondoa kero kwa abiria kutokana na harufu mbaya na kusema kuwa kondakta na dereva ambaye atakamatwa hana sare atatozwa faini ya shilingi elfu 80

Post a Comment

 
Top