Menu
 


Maeneo ambayo hupaki
Madereva wa magari makubwa aina ya malori jijini Mbeya wameilalamikia halmashauri ya jiji kwa kushindwa kuwatengea maeneo maalumu ya kuegesha magari yao licha ya kuendelea kuwatoza ushuru wa uengeshaji wa magari hayo.

Mmoja wa madereva hao Bwana Greyson Mzava amesema mara kwa mara wamekuwa wakiahidiwa kutengewa maeneo ya maegesho lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kutekeleza ahadi zao.

Naye meneja wa wakala wa barabara jijini hapa Bwana Lucian Kiwelo amekanusha malalamiko hayo na kusema kuwa maeneo yametengwa ikiwa ni pamoja na kuwekwa alama za maegesho.

Wakati huohuo amewataka madereva wa magari hayo kutoegesha malori hayo pembezoni mwa barabara ili kutoa nafasi kwa barabara kuendelea kutumika kwa shughuli za usafirishaji.

Post a Comment

 
Top