Menu
 


Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) mkoani Mbeya imewaagiza wasafirishaji wa abiria kutokatisha safari na kwamba adhabu kali itachukuliwa dhidi ya yeyote atakayebainika kukatisha safari zake.Agizo hilo limekuja kutokana na malalamiko ya wakazi wa maeneo ya Isyesye, Uyole na Igawilo kulalamikia tabia ya baadhi ya madereva na makondakta kukatisha safari zao hasa nyakati za jioni.Afisa Mfawidhi SUMATRA kanda ya kusini Bwana Amani Shamaji amesema kitendo kinachofanywa na madereva hao ni kinyume cha kanuni na sheria za usafirishaji na kwamba mamlaka hiyo haitoweza kuvumilia suala hilo.Wakati huohuo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi ama ofisi ya Sumatra ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa dhidi ya Dereva na kondakta mwenye Tabia ya kukatisha safari zake.

Post a Comment

 
Top