Menu
 

 Nembo ya Kikundi cha MBEYA BAMBOO WOMEN

Jengo la Kikundi cha MBEYA BAMBOO WOMEN
Wanawake mkoani Mbeya wameshauriwa kujiunga kwenye kikundi cha umoja wa akinamama cha MBEYA BAMBOO WOMEN GROUP ili waweze kujikomboa dhidi ya ujinga na umasikini.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Pauline Samata amesema katika kikundi hicho wanawake watapata nafasi ya kujifunza shughuli za ujasiriamali ambazo zitawafanya kuondokana katika hali ya utegemezi.

Amezitaja sifa za kujiunga na kikundi hicho kuwa ni elimu ya darasa la saba ambapo wanachama wa kikundi hicho atafundishwa shughuli mbalimbali kama utengenezaji wa vikapu, mikoba, viti, na ufumaji wa masweta ya shule.

Naye mmoja wa wanakikundi hicho Bi.Magreth Zakaria amesema kupitia kikundi hicho amenufaika kupata elimu ya kujitegemea.

Post a Comment

 
Top