Menu
 


Mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini inaziada ya tani milioni 5 za mazao ya Chakula ambazo zitasaidia kulisha mikoa mingine yenye upungufu wa Chakula.Hayo yameelezwa na naibu waziri wa kilimo, chakula na Ushirikika Injinia Christopher Chiza wakati akifungua maonesho ya kilimo nane nane kanda ya nyanda za juu kusini ambayo yanaendelea kufanyika katika viwanja vya John Mwakangale vilivyopo kata ya Isyesye jijini Mbeya.Amesema ziada hiyo ya chakula ni matokeo mazuri yaliyopatikana kutoka kwa wakulima baada ya Serikali kushinikiza wakulima kulima kilimo bora kwa kuzingatia kanuni za kilimo.Aidha amewataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza mkoani Mbeya kwa kufungua viwanda vya usindikaji wa mazao, ambapo kupitia viwanda hivyo wakulima watanufaika kwa kiasi kikubwa katika soko la mazao yao.Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile ameiomba Serikali kuwatafutia wakulima soko la ndani na nje ili waweze kunufaika kupitia kilimo.

Post a Comment

 
Top