Menu
 

Mahudhulio ya wanafunzi wa Shule ya msingi Iganzo jijini Mbeya yamepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia wanafunzi wengi kuzagaa uwanja wa John Mwakangale ambako wanashughulika biashara za kuuza karanga na machungwa pamoja na kusafisha mabanda wakati wa masomo.

Mwalimu wa shule hiyo Bi. Rebeka Kabigi ametoa wito kwa wazazi kuwahimiza watoto wao kwenda shule badala ya kuwaruhusu kwenda kushughulika na biashara hasa msimu huu wa sikukuu za nanenane.

Bi.Jane Masika ambaye ni mmoja wa wazazi alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuwaomba wazazi wenzie kuwahimiza watoto kwenda shule, pamoja na idara ya ulinzi getini kutowaruhusu watoto wa shule kuingia getini muda wa masomo.

Post a Comment

 
Top