Menu
 


RAIA wa Zambia amekutwa amekufa ndani ya Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam, huku watu wengine watatu wakiwa katika hali mbaya kwa kile kinachosemekana kuzidiwa na ulevi. Wanaume hao wanne walikutwa katika chumba namba 425 ghorofa ya nne ndani ya hoteli hiyo iliyoko katikati ya Jiji, watatu wakiwa hawajitambui. Aliyefariki ametambuliwa kwa jina moja la Baster. Habari kupitia chanzo chetu kinasema majira ya saa saba mchana Askari wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, walikutwa wakiendelea na kazi yao huku wafanyakazi wa hoteli hiyo wakionesha wasiwasi kutokana na tukio hilo. Katika mlango wa nyuma wa hoteli hiyo, maiti ya Mzambia huyo ilitolewa na wahudumu wa afya wa kampuni binafsi na kuiingiza katika gari la kampuni hiyo kisha kuondoka nayo chini ya ulinzi wa Polisi.


Post a Comment

 
Top