Menu
 

Maafisa mazingira jiji la Mbeya kesho watafanya ukaguzi wa maeneo ya kata ya Ilomba ambapo faini isiyopungua shilingi elfu kumi itatozwa kwa mwananchi ambaye atabainika kuacha maeneo yake katika hali ya uchafu.

Akiongea na mwandishi wetu mmoja wa wafanyabiashara wa maeneo ya Mama John Geofrey Muhema amesema kitendo cha wafanya biashara kufanya usafi katika maeneo yao kinatokana na agizo lilotolewa na uongozi wa halmashauri la kumtaka kila mtu kufanya usafi katika maeneo yao kabla ya agosti 27 ambayo ndiyo itakuwa siku ya ukaguzi.

Hata hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kujenga mazoea ya kufanya usafi katika maeneo yao badala ya kusubiri amri kutoka kwa viongozi wa Serikali.

Post a Comment

 
Top