Menu
 


Serikali imetenga zaidi ya milioni 5 ili kuimarisha mradi wa maji uliopo kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni moja ya hatua ya kutatua mgogoro baina ya mwekezaji Kapunga Rice Project dhidi ya wakulima wa kijiji hicho.

Hayo yamesemwa bungeni mjini Dodoma na naibu waziri wa mawasiliano na Teknolojia Charles Kitwanga wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mbarali Dickson Kirufi kwa niaba ya Waziri wa kilimo chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe.

Amesema mpango huo utasaida wakulima wa eneo hilo kupata maji kwa ajili ya kumwagilia mashamba yao ya mpunga kwa uhakika bila kuingiliana na mwekezaji wa Kapunga Rice Project.

Ameongeza kuwa mvutano uliopo kati ya mwekezaji na wakulima wa kijiji cha kapunga umechangia kwa kiasi kikubwa na uhusiano mbovu baina ya mwekezaji na wananchi.

Post a Comment

 
Top