Menu
 Nahodha wa timu ya Simba, Juma Kaseja, akipokea na kuibusu Ngao ya Jamii, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo magoli yote yalipatikana kipindi cha kwanza huku goli la kwanza likifungwa na Kiungo wa timu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' na la pili likiwekwa kimiani na Felix Sunzu kwa mkwaju wa penati baada ya Boban kuchezewa faulo eneo la hatari.
Warembo wakibeba Ngao ya Jamii kupeleka jukwaani kwa ajili ya kukabidhi kwa timu mshindi Simba.
Wachezaji wa Simba, wakimbeba mwenzao Patrick Mafisango na kumpongeza baada ya kutangazwa kuwa nyota wa mchezo huo, ambapo alikabidhiwa zawadi na Benki ya NMB.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia huku wakiwa na picha yenye mchoro wa kuwakebehi watani wao wa Jadi Simba, kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
Mashabiki wa Simba, wakishangilia huku wakiburudika na miondoko ya Vuvuzela kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
Winga wa Yanga, Godfrey Taita (kushoto) akijipinda kupiga krosi huku akizuiwa na Patrick Mafisango, wakati wa mchezo huo.
Mchezaji wa Yanga, Hamis Kiiza (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Simba, Nasor Chollo, wakati wa mchezo huo. Kiiza aliingia kipindi cha pili na kufanya mambo makubwa huku akiwanyanyasa mabeki wa Simba akishirikiana na rashid Gumbo, ambapo walionekana kubadilisha kabisa sura ya mchezo huo.
Haruna Niyonzima wa Yanga (kulia) akimtoka beki wa Simba Nasor Chollo.
Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya timu yao kupata bao la kwanza.
Beki wa Simba Victor Costa (kushoto) akimdhibiti, Keneth Asamoh wa Yanga.
Haruna Niyonzima wa Yanga (kushoto) akiwatoka mabeki wa simba wakati wa mchezo huo.
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Simba, Victor Coster.
Tegete, akienelea kumtesa Costa.
Tegete, akijaribu kupenya katikati ya msitu wa mabeki wa Simba....
Boban, akitibiwa nje ya uwanja baada ya kuchezewa faulo iliyozaa penati, lakini katika CHUPA hii aliyoshika mkononi ni aina gani ya kinywaji anakunywa? Tazama kwa makini kisha nipe jibu, sijawahi ona maji yenye rangi hii bwana alaaah!
Kipa wa Yanga Shaban Kado, akijaribu kuokoa mkwaju wa penati iliyopigwa na Felix Sunzu, ambayo hata hivyo ilitinga wavuni na kukataliwa na mwamuzi wa mchezo huo aliyeamuru kurudiwa kwa penati hiyo.
Sunsu na Okwi, wakishangilia baada ya sunsu kufunga kwa penati.
Mashabiki wa Simba wakiwa na furaha ya ushindi.
Jerry Tegete, akiruka kupiga kichwa katikati ya mabeki wa Simba, lakini hata hivyo shuti hilo la kichwa lilipaa juu ya goli.
Hamis Kiiza, akijipinda kupiga kichwa katikati ya msitu wa mabeki wa Simba.
Furaha ya ushindi kwa mashabiki wa Simba.
Hamis Kiiza wa Yanga (kulia) akichuana na beki wa Simba Nasor Chollo.
Kiungo wa Yanga, Rashid Gumbo, akimfinya Amri Kiemba na kumtoka.
Beki wa Simba, Nasor Chollo, akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete.
Boban akichanja mbuga (kulia) ni beki wa Yanga Shadrack Nsajigwa, akipiga hesabu za kumdhibiti.
Hamis Kiiza akiomba dua kabla ya kuingia uwanjani na kuwanyanyasa mabeki wa Simba.
Wachezaji wa Simba wakishangilia. "Raha ya ushindi Bao"........baada ya mchezo huo kumalizika.
Picha zote kwa Hisani ya Sufiani Mafoto

Post a Comment

 
Top