Menu
 


Jengo la kisasa la Benki ya EXIM tawi la Mbeya liliopo Mwanjelwa.
 Taasisi za kifedha nchini zimeanza kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wakulima na wafugaji mkoani Mbeya ili kuwaongezea uwezo katika kilimo.

Meneja wa Exim tawi la Mwanjelwa Bwana Godfrey Kitundu amesema elimu ya huduma hii imetolewa katika wilaya zote za mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuwasaidia wakulima kufaidika na kuwaletea maendeleo kwa kupewa mikopo yenye masharti nafuu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanavikundi kutoka wilaya mbalimbali wamesema kupitia mikopo wameweza kuendesha shughuli zao za kilimo kwa uhakika. 

Post a Comment

 
Top