Menu
 


Zaidi ya wanaume elfu kumi na tisa wamefanyiwa tohara mkoani Mbeya ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya ngono ukiwemo ukimwi.

Hayo yamesemwa na naibu mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa Mbeya Dakta Hemed Kilima ofisini kwake.

Amesema kuwa mpaka sasa zaidi ya wanaume kumi hufanyiwa tohala kila siku ambapo lengo la Serikali ni kuwafanyia Tohara wanaume kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo mpaka sasa wamefikia asilimia 70 kwa mkoa wa Mbeya.

Huduma hiyo ya Tohara kwa wanaume inatolewa bure katika hospitali za Rufaa, hospitali ya wazazi Meta, Igawilo, Tunduma, Hospitali ya Ifisi, Vwawa na hospitali ya Jeshi Mbalizi ambapo kupitia Tohara hiyo wanaume wanakingwa kwa asilimia 60 dhidi ya Ukimwi.

Post a Comment

 
Top