Menu
 

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ameitaka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuacha mara moja kutoza ushuru wa mazao kwa wakulima wadogo ili kuwawezesha kunufaika kupitia kilimo.

PINDA ametoa agizo hilo kufuatia maswali ya msingi yaliyoulizwa na Mbunge Godfrey Zambi na mbunge SAIDI JUMA MKUMBA kuhusu Ushuru wa mazao wanaotozwa wakulima ikiwa ni pamoja na kulazimishwa kuwa na TIN namba kama wafanyabiashara wa muda mrefu.

Kwa mkoa wa Mbeya katika wilaya za Chunya na Mbozi baadhi ya wakulima wamekuwa wakitozwa ushuru wa shilingi elfu 3 hadi tano kwa gunia moja kama ushuru wa mazao yao.

Mmoja wa wakulima wilayani Chunya Bwana Medi Saidi Mwamlima mkulima wa kijiji cha Namkukwe amesema kiwango hicho ni kikubwa na kimekuwa kikichangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya wakulima hapa nchini.

Post a Comment

 
Top