Menu
 

Uchache wa ghuba za kuhifadhia taka katika kata ya Mwakibete mtaa wa Hianga umekuwa kero kwa wananchi waishio maeneo hayo kutokana na halmashauri ya jiji kuchelewa kuzoa taka kwenye ghuba hilo.

 Akiongea Chimbuko Letu na mmoja wa wakazi wa eneo hilo Bi.Aulelia Mwalongo amesema uchafu umekuwa kero kwao na kwamba umekuwa ukisababisha harua mbaya majumbani mwao ikiwa ni pamoja na kuhatarisha afya kwa watoto wadogo.

Ghuba hilo limekuwa likitumia na wakazi wa mitaa ya Mwakibete, njia panda ya Ilomba na Hianga hali inayochangia ghuba hilo kutotosheleza mahitaji ya wakazi wa kata hiyo.

Halmashauri ya jiji kupitia viongozi wa kata na mitaa haina budi kuangalia upya namna ya kuongeza ghuba za taka katika mitaa mbalimbali ili kupunguza kero ya wananchi kukabiliwa na harufu mbaya ikiwa ni pamoja na hofu ya kupatwa na magonjwa ya milipuko.

Post a Comment

 
Top