Menu
 

Baadhi ya wafanyabiashara jijini Mbeya wamekuwa wakishindwa kumudu kuendesha shughuli zao kutokana na kupanda kiholela kwa kodi ya pango la biashara.

Hayo yamebainika kwenye mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa Serikali na wafanyabiashara wa soko la Sido jijini Mbeya.

Akijibu malalamiko yaliyotolewa na wafanyabishara kuhusu tabia ya kupandishwa kwa kodi mara kwa mara inayofanywa na halmashauri ya jiji mkuu wa wilaya ya Mbeya Evansi Balama ameitaka Halmashauri ya jiji kuacha kubadili mikataba hiyo ili kuondoa kero kwa wafanyabiashara.

Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho ofisi yake itakutana na mkurugenzi wa jiji kuangalia namna ya kukabiliana na tatizo hilo lisijirudie.

Post a Comment

 
Top